Loading...
Mkulima mmoja nchini Ufaransa amewashangaza watu ulimwenguni baada ya kuwaandikisha kondoo wake 15 shule ili kufikisha idadi ya wanafunzi inayotakiwa na mamlaka za kijiji kimoja nchini humo.
Ripoti zinasema kuwa, mkulima huyo alichukua hatua hiyo baada ya mamlaka hiyo kutangaza ingeifunga shule ya Jules Ferry iliyopo katika kijiji cha Crêts-en-Belledonne kutokana na idadi ndogo ya wanafunzi.
Kwa mujibu wa ripoti ya jarida la Telegraph la Uingereza, Alhamisi, Mei 9, shule hiyo ya kwenye safu za milima ya Alps karibu na jiji la Grenoble, imekuwa ikikumbwa na tatizo la kushuka kwa idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kila mwaka.
Dundiika News imeng’amua kuwa, kama hatua ya kuzuia mamlaka kuifunga shule hiyo, mkulima mfugaji kwa jina Michel Girerd aliamua kuwasajili baadhi ya kondoo wake kama wanafunzi.
Baadhi ya kwanafunzi hao ambao ni kondoo wanafamika kwa majina kama Baa-bete, Dolly na Shaun ni majina ya baadhi ya kondoo 50 ambao Girerd alifika nao na kuhakikisha wamesajiliwa katika sajili ya shule hiyo, kwenye sherehe maalumu iliyohudhuriwa na watu 200 wakiwemo wanafunzi, walimu na maafisaa wengine.
Baada ya kusajiliwa kwa ‘wanafunzi’ hao, meya wa eneo hilo, Jean-Louis Maret alikabidhiwa vyeti licha ya kuonyesha kusikitishwa sana na tishio la kuifunga shule hiyo kwa sababu ya kukosa wanafunzi wa kutosha.
Baadhi ya walisema mfumo wa elimu hautiliwi maanani hoja zilizopo katika eneo hilo, na badala yake unaangalia tu idadi ya wanafunzi pekee.
“Inasikitisha Elimu ya kitaifa inaangalia tu idadi. Na hivyo sasa, kwa idadi hii, kila kitu ni shwari.” Alisema mzazi mmoja kwa jina Gaelle Laval.
Hadi kufikiwa hatua hiyo wiki jana idadi ya wanafunzi ilikuwa 261 na shule hiyo ina uwezo wa wanafunzi 4,000.
Kwenye sherehe hiyo wanafunzi walibeba mabango yalikuwa na ujumbe: "Sisi si kondoo".
Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

KWELI DUNIA INA MENGI! MKULIMA AWAANDIKISHA KONDOO WAKE SHULE NA KUWAPA MAJINA YA WATU
Reviewed by By News Reporter
on
5/11/2019 09:25:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: