Loading...

MCHUNGAJI FEKI AFUMANIWA AKIPANDIKIZA UCHAWI KATIKA NYUMBA ILIYOKARIBU NA KANISA LAKE

Loading...
Kioja kilishuhudiwa eneo la Maungu, Voi Kaunti ya Taita - Taveta nchini Kenya baada ya pasta mmoja bandia kufumaniwa akifinya ushirikina katika nyumba ya jirani yake. 

Kulingana na aliyeshuhudia kisa hicho ambaye alizungumza na jarida moja la habari la nchini humo, 'mtumishi' huyo wa Mungu alifumaniwa Ijumaa, Mei 24 akichimba na kupandikiza vifaa vyake vya kichawi katika nyumba yaa mama mmoja akidai kuwa alikuwa akijiandaa kutoa mapepo.

Pasta huyo alinusurika kichapo cha mbwa koko lakini aliokolewa na maafisa wa polisi tawala waliokuwa wakipiga doria na kuitwa haraka kuwatuliza wakazi waliokuwa na hasira. 

Inadaiwa mhubiri huyo bandia alipatikana na vifaa vya ajabu likiwamo jeneza dogo, hirizi, damu iliyokuwa kwenye chupa na vitu vingine vinavyotumiwa na washirikina.

Kulingana na mdokezi aliyezungumza na jarida hilo la TUKO, visa vya ubakaji wa watoto na hata mbuzi eneo la Maungu vimekuwa vikishuhudiwa lakini mhusika amekuwa akiwakwepa kwa muda mrefu na sasa wanashuku mhusika huyo ni pasta huyo bandia. 

"Tumechoka na visa hivi, juzi hapa hapa kijijini kuna jamaa ameamka na kumkuta mbuzi wake amefanyiwa kitendo cha ajabu," alisema mmoja wa wakazi ambaye hakutaka jina lake kutajwa. 

Polisi walimchukua mshukiwa huyo na vifaa vyake na sasa anazuiliwa huku uchunguzi zaidi ukiendelea kabla ya hatimaye kufikishwa kortini ikiwa atapatikana na hatia.
Na Yohana Musa.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MCHUNGAJI FEKI AFUMANIWA AKIPANDIKIZA UCHAWI KATIKA NYUMBA ILIYOKARIBU NA KANISA LAKE MCHUNGAJI FEKI AFUMANIWA AKIPANDIKIZA UCHAWI KATIKA NYUMBA ILIYOKARIBU NA KANISA LAKE Reviewed by GEOFREY MASHEL on 5/26/2019 08:27:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.