Loading...

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA 'MAY' ATHIBITISHA KUJIUZULU, KUONDOKA OFISINI RASMI JUNI 7

Loading...
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amejiuzulu kutoka wadhifa huo na kutangaza kutoa nafasi ya kuchaguliwa kwa waziri mkuu mpya wa Uingereza. 

May anajiuzulu hata baada ya kufeli kuafiki mchakato wa Uingereza kujiondoa katika umoja wa Ulaya maarufu kama Brexit.

Kwenye taarifa yake iliyoibua hisia mseto katika eneo la Downing Street, Bi May alidokeza kuwa amejikakamua na kufanya kila awezalo ili kuafiki kura za maoni kuhusu EU ya mnamo 2016, BBC iliripoti. 

Alisimulia majuto yake kwa kushindwa kutimiza swala hilo nzito la Brexit akiongeza kuwa alikuwa na imani waziri mkuu mpya atakayeteuliwa atawapa wananchi suluhu ambayo wamekuwa wakiisubiri kwa muda.

"Nimejaribu niwezavyo kuwarai wabunge kuunga mkono mchakato huo, lakini juhudi zangu ziligonga mwamba," May alisema. 

Akiwa mwingi wa hisia wakati akitoa tangazo lake, May alifichua kwamba alifanya uamuzi huo kama njia moja ya kuheshimu sauti ya wengi nchini humo.

"Natangaza kujiuzulu kama kiongozi wa chama cha Conservative ifikiapo Ijumaa, Juni 7. Natoa fursa ya kuidhinishwa mchakato wa kuchaguliwa waziri mkuu mpya Uingereza," taarifa ya May ilidokeza. 

Bi. May atasalia kuhudumu kama waziri mkuu hadi Juni 7 pale ambapo kiongozi mpya wa chama cha Conservative atakapochaguliwa.
Na Geofrey Okechi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WAZIRI MKUU WA UINGEREZA 'MAY' ATHIBITISHA KUJIUZULU, KUONDOKA OFISINI RASMI JUNI 7 WAZIRI MKUU WA UINGEREZA 'MAY' ATHIBITISHA KUJIUZULU, KUONDOKA OFISINI RASMI JUNI 7 Reviewed by GEOFREY MASHEL on 5/26/2019 08:39:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.