Loading...
Mchimbaji mdogo wa madini mkoani Shinyanga ameibuka na kuwa bilionea ghafla baada ya kuuza almasi yake kwa takriban dola milioni moja nukta nne sawa na Tsh. Bilioni 3.
Almasi hiyo yenye karati 512 ilipatikana na mchimbaji madini mdogo Joseph Temba wiki mbili zilizopita katika eneo la Maganzo huko Shinyanga.
Bwana Temba ameishukuru Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwa muongozo na usimamizi wa Almasi yake na muongozo wa utaratibu wa mauzo ambao uko wazi.
Ametoa wito kwa wachimbaji wadogo wezake kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali kwani kuna faida nyingi hivyo hawana sababu ya kukwepa Masoko hayoo.
Kulingana na naibu waziri wa madini nchini humo Stanlaus Nyongo almasi hiyo ndio kubwa zaidi kuwahi kupatikana nchini humo.
Akifichua tangazo la kupatikana kwa almasi hiyo katika mtandao wake wa Twitter bwana Nyong'o alisema kuwa serikali imejipatia shilingi milioni 238 kutokana na mauzo ya madini hayo.
Nyongo amewahimiza na kuwasisitizia wachimbaji wote na wanunuzi kote nchini kufanya shughuli hizo kwenye masoko ya madini yaliyoainishwa na kutambulika na Serikali.
Amempongeza bwana Joseph Temba kwa kufuata utaratibu katika mauzo yake na kwamba Serikali itaendelea kusimamia mauzo yake mpaka hatua ya mwisho.

Na Ummy Boaz.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
TANZANIA YAPATA BILIONEA MPYA
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
5/27/2019 06:41:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: