Loading...

MWANAUME MZEE ZAIDI DUNIANI AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 123

Loading...
Mwanamume anayedai kuwa mtu mzee zaidi duniani ameripotiwa kuaga dunia akiwa na miaka 123.

Kulingana na ripoti ya Daily Mail, raia huyo wa Urusi kwa jina Appaz Iliev, alikuwa mzaliwa wa jamhuri ya Ingushetia, karibu na Georgia, na alizaliwa wakati wa utawala wa mwisho wa Tsar nchini humo.

Iliev ambaye hadi kifo chake alikuwa na watoto wanane, wajukuu 35 na vitukuu 34 pia alifichua kuwa, alishiriki vita vya Dunia vya Kwanza na alipoambiwa ni mzee sana kupigana vita, aliishi akiwa mchungaji kondoo. 

Ripoti hiyo pia ilisema kuwa, stakabadhi za kuzaliwa za Iliev zilipotea na umri wake kamili haungethibitishwa, na kuongeza kuwa mtu mzee zaidi ambaye umri wake ulithibitishwa ni Mmarekani kwa jina Sarah Knauss.

Kuhusu alivyofanikiwa kuishi miaka mingi kiasi hicho, iliripotiwa kuwa alisema alitumia saa 11 kulala kila usiku, na kuingia kwake kitandani kulikuwa 7pm na kuamka 6am kuchunga kondoo wake. Pia alisema alikoma kuhudumiwa na madaktari na dawa ingawa katika umri wa miaka 121, alifanyiwa upasuaji. 

Mlo wa Iliev ulikuwa samaki na mboga kutoka shamba lake na nyama iliyochinjwa kijijini kwao Guli, katika milima ya Caucasus. Alikunywa maziwa na maji safi kutoka kisimani.
Na Timoth Jacob.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MWANAUME MZEE ZAIDI DUNIANI AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 123 MWANAUME MZEE ZAIDI DUNIANI AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 123 Reviewed by By News Reporter on 5/16/2019 09:55:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.