Loading...

POGBA AIBUKIA MECCA BAADA YA EPL KUMALIZIKA

Loading...
Mchezaji staa wa klabu ya Manchester United, Paul Pogba amewasili mji mtakatifu kwa imani ya dini ya Kiislamu wa Mecca katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 

Baada ya kutua mji huo, Pogba mwenye umri wa miaka 26, alionekana akiwa karibu kabisa na al-Ka bah ambayo ipo Saudi Arabia.

Mchezaji huyo amekuwa muhimu sana katika timu yake na kuonekana kwake Mecca kunajiri mara baada ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu ya England ambapo timu yake ilimaliza katika nafasi ya sita. 

Katika moja ya picha zake alizoichapisha Instagram, Pogba akiwa mji huo mtakatifu, aliandika ujumbe muruwa wa kuwausia mashabiki wake.

”Kamwe usisaha vitu muhimu katika maisha” aliandika. 

Tukio hili sio la kwanza kwa Pogba ambaye ni raia wa Ufaransa, kwani katika misimu miwili iliyopita mchezaji huyo alitembelea mji huo mtakatifu. 

Msimu uliokamilika mwishoni mwa juma lililopita, Pogba alipitia wakati mgumu sana kufuatia kutupiwa matusi na mashabiki waliochukizwa na matokeo mabaya ya klabu hiyo.

Itakumbukwa kuwa, United walikubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Cardiff katika uwanja wa Old Trafford. 

Sasa mchezaji huyo anahusishwa na Real Madrid huku duru zikisema, meneja wa klabu hiyo Zinedine Zidane anamsaka kufa kupona.
Na Mussa Rashid.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
POGBA AIBUKIA MECCA BAADA YA EPL KUMALIZIKA POGBA AIBUKIA MECCA BAADA YA EPL KUMALIZIKA Reviewed by By News Reporter on 5/18/2019 09:09:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.