Loading...

TAFITI: WALEVI KUONGEZEKA, KILA SEKUNDE 10 WATU HUFA KWA POMBE

Loading...
MATUMIZI ya pombe yanatarajiwa kuongezeka duniani kwa muongo ujao kutokana na nchi mbalimbali kutotelekeza ahadi ya kuwalinda wananchi wao kutoka katika matumizi mabaya ya vilevi.

Tafiti zinaeleza kuongezeka kwa matumizi ya pombe kimataifa yanachangia ongezeko la matumizi hayo ya pombe kwa nchi zenye vipato vya chini. 

Taasisi ya Kimataifa ya IOGT, imebainisha kuwa matokeo ya utafiti uliopita yalionesha kuwa malengo ya kupunguza matumizi hatari ya pombe hayawezi kufikiwa endapo hatua za haraka za kudhibiti matumizi hayo hazitachukuliwa.

Ripoti nyingine ya dunia ya matumizi ya pombe iliyochapishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ya Septemba mwaka jana, inaonesha jinsi pombe inavyoathiri malengo mengi ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ikiwemo ya kutoa ahadi ya kujenga jamii yenye usawa na iliyo bora.

Taasisi hiyo iliweka wazi na kufafanua kuwa ni lazima serikali kuhakikisha kuwa wanachukua hatua za haraka za kudhibiti matumizi ya pombe, kutekeleza sera bora za kudhibiti pombe na kutimiza ahadi ya kulinda watu kutoka katika madhara ya matumizi hayo na kufikia afya na maendeleo kwa wote. 

Hata hivyo, matumizi hayo ya pombe duniani yanakadiriwa kuua watu milioni 3.3 kila mwaka ikimaanisha kuwa kila baada ya sekunde 10 watu hufa kwa sababu ya pombe. 

Pia inakadiriwa vijana kati ya miaka 20 hadi 39, sawa na asilimia 25 hufa kutokana na matumizi ya pombe ikiwa ni sawa na asilimi 5.9 ya vifo vyote.
Na Vicky Paul.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
TAFITI: WALEVI KUONGEZEKA, KILA SEKUNDE 10 WATU HUFA KWA POMBE TAFITI: WALEVI KUONGEZEKA, KILA SEKUNDE 10 WATU HUFA KWA POMBE Reviewed by By News Reporter on 5/18/2019 08:50:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.