Loading...

JWTZ WAENDA SUDAN KULINDA AMANI, WATUMIA DREAMLINER YA ATCL

Loading...
WANAJESHI kadhaa wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania (JWTZ) wameondoka kwenda Sudan kulinda amani kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Wanajeshi hao kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka 12 ya ushiriki wa Tanzania kwenye ulinzi wa amani Sudan, wamesafirishwa kwa kutumia ndege ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Boeing 787- 8 Dreamliner. Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa JWTZ, Meja Jenerali Alfred Kapinga alisema kusafirisha wanajeshi hao kwa kutumia ndege ya ATCL ni uzalendo wa hali ya juu kwa nchi.

Alisema; ” leo tunawaaga wanajeshi wetu wanaokwenda kulinda amani Sudan, wanajeshi hawa wana mafunzo na weledi wa hali ya juu katika ulinzi wa amani, kwanza wana nidhamu na uelewa wa kazi lakini kikubwa zaidi na cha kujivunia wanakwenda kwa kutumia usafiri wetu wenyewe wa ndege. “Awali tulikuwa tunatumia usafiri wa mashirika mengine ya ndege ambayo yalikuwa yakiwapeleka wanajeshi wetu nchi mbalimbali kulinda amani, lakini leo kwa mara ya kwanza tangu tumeanza kwenda kulinda amani Sudan, tumetumia ndege yetu ya nyumbani, hii ni hatua nzuri sana.”

Alisema, pamoja na kuwasafirisha kwa mashirika ya ndege ye nje ya nchi lakini pia walikuwa wakitumia ndege za kijeshi lakini kwa ubora wa ndege za ATCL za hivi sasa, wanajeshi hao watasafirishwa kwa ndege hiyo ya ATCL kwenda na kurudi. Pia Meja Jenerali Kapinga alibainisha kuwa kwa kuwasafirisha wanajeshi kwa ndege za hapa nchini kunawaongezea ari ya uzalendo na uhakika wa usalama wao kutokana na imani yao kuwa wanasafirishwa kwa kutumia chombo cha nyumbani hadi kwenye eneo lao la kazi.

Aliongeza kuwa wanajeshi wa Tanzania wamekuwa wakifanya kazi ya ulinzi wa amani kwa nguvu zao zote na kwa kuzingatia miiko inayotakiwa na ndio maana Umoja wa Mataifa (UN) umekuwa ukiitumia nchi ya Tanzania kwenye shughuli nyingi za ulinzi wa amani. Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi alishukuru JWTZ kwa uamuzi wake wa kuishauri UN kutumia ndege ya ATCL kwa ajili ya kusafirisha wanajeshi.

Alisema,”pongezi zetu nyingi kwa Mkuu wa Majeshi na jeshi zima kwa kuamua kuwasafirisha wanajeshi wetu kwa kutumia ndege yetu, hakika ni hatua kubwa ya mafanikio.” Mmoja kati ya wanajeshi wanaokwenda kulinda amani Sudan, Wilfrida Sabath alisema kuwa wamejipanga kwenda kulinda amani na kurejea nyumbani salama huku akipeleka pongezi kwa Rais John Magufuli kwa kununua ndege hiyo iliyowawezesha kusafiria kwenda Sudan.
Na Geofrey Okechi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JWTZ WAENDA SUDAN KULINDA AMANI, WATUMIA DREAMLINER YA ATCL JWTZ WAENDA SUDAN KULINDA AMANI, WATUMIA DREAMLINER YA ATCL Reviewed by By News Reporter on 5/18/2019 08:32:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.