Loading...

KIWANDA CHA KUCHAKATA KOROSHO KUJENGWA MTWARA

Loading...
WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema serikali inajenga kiwanda cha kuchakata mazao ya korosho (mabibo) ili kuzalisha, kutengeneza juisi na mvinyo Naliendele Mtwara.

Waziri Hasunga alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ndanda, Cecily Mwambe (Chadema), aliyetaka kujua utafiti wa kuongeza thamani mazao ya korosho (mabibo) umefikia wapi na lini juisi na mvinyo zitaanza kutengenezwa katika Kituo cha Utafiti Kilimo cha Naliendele (NARI) Mtwara.

Hasunga alisema ni kweli utafiti wa kina ulifanyika kuhusu namna ya kuongeza thamani mazao ya korosho (mabibo) ili kutengeneza juisi na mvinyo na maagizo yaliyopo ni kujenga kinu cha kuchakata mazao hayo ili kutengeneza vinywaji hivyo.
Na Ummy Zuberi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KIWANDA CHA KUCHAKATA KOROSHO KUJENGWA MTWARA KIWANDA CHA KUCHAKATA KOROSHO KUJENGWA MTWARA Reviewed by By News Reporter on 5/18/2019 08:20:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.