Loading...
Kuimarika kwa udhibiti wa shughuli za madini na kuongezeka kwa uzalishaji miongoni mwa wazalishaji katika migodi mikuu, hususan ile ya Geita na North Mara, kumeinua mapato yatokanayo na uuzaji wa nje wa madini ya dhahabu kwa Tanzania.
Kwa mujibu wa tathmini ya uchumi ya mwezi ya Benki kuu ya Tanzania (BoT) ya mwezi April, mapato yatokanayo ya uuzaji wa dhahabu yameongezeka kwa $100 milioni (takribani Sh223 bilioni) mwishoni mwa mwaka uliomalizika Machi, mwaka huu, ikilinganishwa na mwaka uliomalizika Machi, 2018.
Tathmini hiyo inaonyesha kuwa mapato yanayotokana na mauzo ya nje ya dhahabu yameongezeka kwa kiwango cha dola bilioni 1.68 katika mwaka uliomalizika mwezi Machi mwaka huu, kutoka dola bilioni $1.53 kiwango kilichorekodiwa wakati wa mwaka uliomalizika Machi 2018.
BoT inasema kuwa uuzaji wa bidhaa nyingine katika nchi za nje umeongezeka,
na mafanikio haya yametokana na kuongezeka kwa thamani ya bidhaa na huduma zilizouzwa nje ya nchi katika mwaka uliomalizika Machi 2019 hadi dola bilioni $8.5 kutoka dola bilioni $8.4 katika kipindi kama hicho hicho kilichomalizika 2018.
Hata hivyo haya yanaripotiwa huku bei ya bidhaa hiyo ikiendelea kushuka kila mwezi ,ripoti inaonyesha kuwa bei ya dhahabu pia ilianguka kwa asilimia 1.5 hadi $1,300.9 mwezi Machi mwaka huu kutoka $1,320.1 mnamo mwezi Februari mwaka huu.
Katibu mkuu mtendaji wa tume ya madini , Prof Shukrani Manya, alisema kuwa kupitishwa kwa sheria tatu mwaka 2017 kumeathiri ukuaji wa sekta hiyo.
Mafanikio haya katika sekta ya madini nchini Tanzania yanakuja baada ya Dkt John Pombe Magufuli kumteua Profesa Shukurani Elisha Manya kuwa Kamishna wa Madini ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini nchini baada ya kumfuta kazi Kamishna aliyekuwepo Mhandisi Benjamin Mchwampaka.
Manamo mwaka 2017, bunge la Tanzania lilipitisha mabadiliko ya sheria tatu zilizoleta mabadiliko makubwa ya kisheria na mfumo wa taasisi zinazoongoza sekta ya mafuta, gesi na uzalishaji wa madini.

Na Yuda Kanuti.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SEKTA YA MADINI YAULA, FAIDA KEDEKEDE MAUZO YA NJE YA DHAHABU
Reviewed by By News Reporter
on
5/14/2019 08:54:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: