Loading...
Kuna mambo mengi yana mchango mkubwa katika maisha yetu lakini wengi bado tunashindwa kuyafanya. Ukiangalia hakuna sababu ya msingi kwa nini hatufanyi mambo hayo.
Mara nyingi tunaogopa kuchukua hatua fulani hadi pale tutakapo pata uhakika kuwa tunaweza kulifanya jambo hilo kwa usahihi. Tukitaka kuchukua hatua huwa kunakuwa na sauti kutoka ndani ambayo inatuambia bado hatuna uwezo na hutuwezi kufanya vizuri. Wengi wanatii sauti hii na kuendelea kusubiri hadi pale watakaporidhika kuwa wana uwezo wa kufanya kwa usahihi katika kiwango cha juu.
Sauti hizi zimekwamisha watu wengi sana, wameendelea kutii sauti hizi na siku zote wameendelea kusubiri bila kufanya chochote. Hadi leo hii wanaendelea kusubiri bila kushtuka kuwa wamedanganywa. SIRI ni kutotii sauti yoyote inayokuambia bado huna uwezo.
Ukitaka kupambana na sauti hizi wewe anza kufanya hivyo hivyo hata kama utafanya vibaya na kuharibu. Kitendo cha wewe kuanza tu kitakuwa ni ushindi dhidi ya ile sauti iliyokuwa inakuzuia na utaendelea kuchukua hatua katika hali hiyo hiyo na mbele ya safari utazidi kuboresha zaidi na kurekebisha makosa. Baada ya muda utajifunza na kuanza kufanya vizuri katika kiwango bora.
Mara nyingi watu hatuchukui hatua kwa sababu hatuna uhakika kama tunaweza kufanya vizuri, hakuna namna utapata uhakika huo zaidi ya kujaribu na kuanza hivyo hivyo.
Keep Moving ! One Step At A Time !!
Vicent Stephen

Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SIRI YA UTAJIRI: KWANINI HATUFANYI MAMBO YA MSINGI KATIKA MAISHA YETU?
Reviewed by By News Reporter
on
5/22/2019 11:09:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: