Loading...

WANASIASA WA UPINZANI NA WENYE NGUVU ZAIDI WAUNGANA KUMNG'OA MUSEVENI

Loading...
Mbunge wa upinzani nchini Uganda ambaye pia ni msanii wa muziki, Robert Kyagulanyi  maarufu kama Bobi Wine ameungana na mwanaharakati wa kisiasa Dkt. Kizza Besigye wameahidi kushirikiana kukiondoa madarakani chama tawala National Resistance Movement (NRM) kinachoongozwa na rais Yoweri Museveni.

Taarifa iliyotolewa na wawili wapinzani hao wenye nguvu zaidi nchini Uganda, imeeleza kuwa baada ya mazungumzo kati yao, wamekubaliana kuhusu masuala kadhaa wakati wanapokuja pamoja kushirikiana kisiasa dhidi ya rais Museveni kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka 2021.

Hapo jana akizungumza na waandishi habari, Bobi Wine alisema wamekuwa wakishauriana katika mikutano kadhaa na vyama tofuati vya kisiasa nchini kikiwemo cha Democratic Party maarufu DP bloc na hivi karibuni na kiongozi wa People’s government, Dkt Kizza Besigye.


Bobi yeye hana Chama ni mgombea huru na kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Kyadondo, Na Chama tawala cha NRM kinachoongozwa na Rais Museveni kimekuwa madarakani tangu 1986.
Na Geofrey Okechi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WANASIASA WA UPINZANI NA WENYE NGUVU ZAIDI WAUNGANA KUMNG'OA MUSEVENI WANASIASA WA UPINZANI NA WENYE NGUVU ZAIDI WAUNGANA KUMNG'OA MUSEVENI Reviewed by By News Reporter on 5/09/2019 07:50:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.