Loading...

ALIKIBA: HATA NIKIWA NA WALINZI 100 HAISAIDII KITU, MTU AKITAKA KUNIUA ANANIUA TU

Loading...
Nyota wa nyimbo za bongo fleva,  Mfalme Ali Kiba amesema hana pesa za kuwalipa walinzi kwani anaamini Mungu ndiye mwenye kutoa uhai na ndiye anayemlinda kwa vyovyote vile.

Wengi wa wanamuziki wenzake akiwemo Diamond Platinumz na Harmonize huonekana kila mara hasa wakienda kwenye tamasha lolote wakiwa wamezingirwa na walinzi kadhaa. 

Kulingana na Kiba mtu yeyote anaweza akauwawa hata akiwa na walinzi na kwake yeye haamini kulindwa na binadamu.

"Akikulinda Mungu inatosha ila wale wenye ustaa wanataka wawe na walinzi kama rais na hata wengine wamepata pesa hivi majuzi," Kiba alisema akiwa kwenye mahojiano na mtandao wa YoFave. 

"Hata nikiwa na walinzi zaidi ya 100, haisaiidii chochote, mtu akitaka kuniua ataniua tu, mimi sihitaji walinzi kwa kuwa nalindwa na Mungu," Kiba aliongezea.
Na Haika Gabriel.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
ALIKIBA: HATA NIKIWA NA WALINZI 100 HAISAIDII KITU, MTU AKITAKA KUNIUA ANANIUA TU ALIKIBA: HATA NIKIWA NA WALINZI 100 HAISAIDII KITU, MTU AKITAKA KUNIUA ANANIUA TU Reviewed by GEOFREY MASHEL on 6/12/2019 08:35:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.