Loading...

EBOLA ILIVYOIBUKIA UGANDA, WAZIRI UMMY ASEMA NENO

Loading...
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewatoa hofu Watanzania kufuatia Shirika la Afya Duniani (WHO) kuthibitisha ugonjwa wa Ebola kuingia nchini Uganda.

Juni 6, 2019 shirika hilo lilibaini mgonjwa wa Ebola nchini humo Uganda.

Jana Jumatano Juni 12, 2019 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Ummy ameandika ujumbe wa kuwatoa hofu Watanzania, akiwataka kuwa watulivu wakati Serikali ikijipanga kutoa taarifa rasmi.

Amesema Wizara ya Afya imeanza kuchukua tahadhari kukabiliana na ugonjwa huo.

Aliandika: "Tumepokea kwa Tahadhari kubwa uwepo wa ugonjwa wa #Ebola nchini Uganda. Serikali kupitia Wizara ya Afya imekuwa ikichukua hatua za utayari (preparedness) wa kukabiliana na ugonjwa huu. Wananchi wasiwe na hofu. Tutatoa Taarifa zaidi kwa umma ktk siku chache zijazo."
Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
EBOLA ILIVYOIBUKIA UGANDA, WAZIRI UMMY ASEMA NENO EBOLA ILIVYOIBUKIA UGANDA, WAZIRI UMMY ASEMA NENO Reviewed by By News Reporter on 6/13/2019 09:23:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.