Loading...

FACEBOOK KUJA NA PESA YAO YA KIDIGITALI 'LIBRA' KUANZIA 2020

Loading...
Mtandao wa kijamii wa Facebook umetangaza kuingiza sokoni pesa mpya ya kidigitali sokoni.

Tangazo hilo kutoka Facebook linasema pesa hiyo mpya ya kidigitali itayoingizwa sokoni mwaka 2020 itaitwa “Libra”.Pesa hiyo pia itakubalika katika mifumo ya malipo kama vile Visa na Mastercard.

Taarifa hiyo inasema baada ya kuingizwa sokoni pesa hiyo ya kidigitali itaanzishwa pia pochi ya kidigitali ya kuhifazia pesa hio iitwayo “Calibra”. Taarifa hiyo inasema huduma hiyo kwa watumiaji itawezesha kuokoa pesa pia matumizi na kutumiana pesa miongoni mwao.

Katika taarifa hiyo ya Facebook imekumbushia kwamba pesa hiyo ya kidigitali na pochi ya kidigitali vitaweza kutumiwa na mtu yeyote ambaye kwenye simu yake ila awe na programu tumizi za  Facebook Messenger, WhatsApp au “Calibra”.
Na Yohana Samweli.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
FACEBOOK KUJA NA PESA YAO YA KIDIGITALI 'LIBRA' KUANZIA 2020 FACEBOOK KUJA NA PESA YAO YA KIDIGITALI 'LIBRA' KUANZIA 2020 Reviewed by By News Reporter on 6/21/2019 08:17:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.