Loading...
1. JIFUNZE KUKUMBUKA MAJINA YA WATU. Sio kila mtu anapenda aitwe “wee kaka/dada”, “ankoo”, “mzee”. Kukumbuka majina ya watu sio tu itakupa heshima, bali pia utaonekana ni mtu makini na unayejali.
2. Msifie mtu anapofanya kitu au jambo zuri (compliments). Nani hapendi kusifiwa?
3. Jifunze namna ya kufikisha habari mbaya/ ya kusikitisha kama msiba, ajali n.k
4. Usipende kuangalia saa unapoongea na mtu. Hasa anapokuelezea tatizo lake. Badala yake kama unaona anakuchelewesha, tengeneza mazingira ya kupigiwa simu ili uondoke.
5. Jifunze Kutabasamu unapopigwa picha, Ina maana kubwa sana.
6. Jifunze kuepuka ugonvi. Na ukiingia kwenye Ugonvi kwa bahati mbaya basi jifunze kushuka la sivyo hakikisha unashinda ugonvi huo.
7. Jifunze kuwa msikilizaji mzuri. Kumbuka, Kila mtu anapenda kusikilizwa.
8. jifunze kusema samahani na ahsante. Epuka kutumia maneno kama “najua” au “mimi pia”badala yake elezea unajua kiasi gani badala ya kutumia maneno hayo moja kwa moja.
9. Jifunze kuonyesha unakumbuka matatizo ya watu waliyokueleza hapo hawali na usisahau kuwauliza wamefikia wapi mnapokutana. Mfano kama alisema ana mgonjwa basi kumbuka kumuuliza hali ya mgonjwa. Kumbuka binadamu tunapenda kuonewa huruma.
10. Jifunze namna ya kumuonyesha ukarimu mgeni. Pia jifunze kuwa mgeni bora pale unapokaribishwa na mwenyeji wako

Na Haika Gabriel.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JE UNAHITAJI KUKUBALIKA NA KILA MTU? JIFUNZE KUFANYA MAMBO HAYA
Reviewed by By News Reporter
on
6/25/2019 06:57:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: