Loading...

JESHI LA WANANCHI LATANGAZA KIAMA KWA VIONGOZI

Loading...
JWTZ yatangaza kiama kwa Viongozi walioshiriki kufanya udanganyifu zoezi la kujiunga na Jeshi kwa ajili ya kujitolea.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limetangaza kiama kwa Viongozi walioshiriki kufanya udanganyifu katika zoezi la uanadikishaji wa vijana wa kujiunga na jeshi kwa nafasi za kujitolea linaloendelea Nchini ambapo imebainika kuwa baadhi ya vijana wamefoji vyeti vyao mbalimbali na huku baadhi ya viongozi wakishiriki kuomba nafasi hizo kinyume cha taratibu.

Taarifa hiyo imetolewa na Luteni Kanali Gaudence Ilonda ambaye ni Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi hilo, ambapo amesema kuna matatizo mbalimbali yamejitokeza wakati wa zoezi hilo,  ambapo jeshi imeshindwa kuzifumbia macho ikiwemo baadhi ya vijana kujiandikisha katika mikoa ambayo hawaishi huku wengine wakitoa taarifa za Uongo.

''Baadhi ya viongozi wamekuwa wakileta majina kuwaombea ndugu, jamaa au marafiki  nafasi za Jeshi hapa Makao Makuu, na wengine huko Mikoani hao vijana wamechujwa na nani/? kama si kutengeneza vikundi? kwa ajili ya Matumizi yao Binafsi?

 Kuna changamoto imeota mizizi na tunataka kuikata ambayo ni suala la utapeli na Jeshi hatuna utaratibu huo.

''Tunakusudia kufanya zoezi kabambe la kupitia upya vijana wote watakaokuwa wameandikishwa kutoka katika mikoa yote, wengine wamefoji hata Afya, hivi sasa tumeandaa jopo la Madaktari watakaowapima upya , kazi ya jeshi inahitaji utimamu wa mwili na mawazo na kupitia Upya Nyaraka na Vyeti vyote.

Zoezi hilo litashirikisha sekta Mbalimbali ikiwemo Wizara ya Elimu, Takukuru,Jkt, NIDA na kwamba watakaobainika wamefoji watakamatwa na kuchukuliwa hatua sitahiki.
Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JESHI LA WANANCHI LATANGAZA KIAMA KWA VIONGOZI JESHI LA WANANCHI LATANGAZA KIAMA KWA VIONGOZI Reviewed by GEOFREY MASHEL on 6/28/2019 06:32:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.