Loading...
Kisukari NININI? Kisukari ni ugonjwa unaotokana namtu kuwa na sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu. Ugonjwa huo huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembe kutoka kwenye damu kwa kuwa chembe huhitaji sukari ili kupata nishati.
Matokeo ni kuharibiwa kwa viungo muhimu na hitilafu ya mzunguko wa damu, na nyakati nyingine unaweza kufanya mtu akatwe vidole vya miguu au mguu, pia husababisha upofu, na maradhi ya figo. Wagonjwa wengi wa kisukari hufa kutokana na mshtuko wa moyo au kiharusi.
DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI:
1. Kiu iliyozidi
2. Kukojoa mara kwa mara
3. Kupatwa na ganzi kwenye miguu na mikono
4. Kujisikia mchovu
5. Kutoona vizuri
6. Kuongezeka njaa
7. Kushindwa kuhimili tendo la ndoa
JINSI YA KUEPUKA KISUKARI:
i) Pimwa kiwango cha sukari kwenye damu ikiwa una uwezekano mkubwa wa kupata kisukari.
ii) Kula vyakula vyenye lishe. Unaweza kufaidika ukifanya mambo yafuatayo: Punguza kiasi cha chakula unachokula. Badala ya kunywa vinywaji vyenye sukari nyingi au vinywaji vyenye kaboni kama vile soda, kunywa maji, chai, au kahawa. Kula vyakula vya nafaka ambayo haijakobolewa badala ya vyakula vilivyochujwa sana viwandani. Kula nyama isiyo na mafuta mengi, samaki, njugu, karanga, na maharagwe.
iii) Fanya mazoezi. Kufanya mazoezi kunaweza kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu na kukusaidia uwe na uzito unaofaa. Mtaalamu fulani anapendekeza kupunguza muda unaotumia kutazama televisheni ili uwe na muda wa kufanya mazoezi.Huwezi kubadili chembe zako za urithi, lakini unaweza kubadili maisha yako. Utafaidika sana ikiwa utajitahidi kutunza afya yako.

Na Geofrey Okechi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
ZIJUE DALILI NA MADHARA YA KISUKARI NA JINSI YA KUEPUKA
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
6/28/2019 06:57:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: