Loading...

JOTO ULAYA LIMEKUWA TISHIO, AFRIKA YAHUSIHWA KAMA NI CHANZO

Loading...
Bara la Ulaya limeathiriwa vibaya na wimbi la joto linalosemekana kutokea Kaskazini mwa Afrika.

Joto linatarajiwa kuongezeka katika nchi nyingi barani Ulaya katika siku tatu  zijazo.

Katika nchi zingine,kutokana na joto ambalo limevunja rekodi , wataalam, wamewaasa wazee, watoto na wanawake wajawazito kutotoka nje.

Hali ya hewa ya joto inatarajiwa kuathiri nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Hispania na Ujerumani.

Nchini Ufaransa, wastani wa joto ulifikia 34.9 jana na kuvunja rekodi tangu 1952. Leo, joto limefikia 34 katika jiji la Paris.

Joto kali limeathiri hasa maeneo ya kusini mwa Ufaransa.

Hali ya joto imesababisha mitihani iahirishwe mashuleni nchini Ufaransa.

Uchafuzi wa hali ya hewa nao umeikumba nchi hiyo.

Kutokana na wimbi la joto linaloathiri nusu ya Hispania,joto limeripotiwa kufikia nyuzijoto 42 .

Ujerumani imefikia kiwango cha 38.6 na kuvunja rekodi tangu 1947.

Watu wawili wamepoteza maisha nchini Italia ndani ya masaa 24  yaliyopita.

Mwishoni mwa juma, kwa sababu ya joto lenye kufikia digrii 43, miji 19 ikiwa ni pamoja na Roma, Firenze na Perugia zimetoa tahadhari kwa wananchi.
Na Lameck Ditto.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JOTO ULAYA LIMEKUWA TISHIO, AFRIKA YAHUSIHWA KAMA NI CHANZO JOTO ULAYA LIMEKUWA TISHIO, AFRIKA YAHUSIHWA KAMA NI CHANZO Reviewed by By News Reporter on 6/29/2019 06:59:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.