Loading...

MAELFU WAANDAMANA KUTAFUTA USAWA KUHUSU USHOGA

Loading...
Maelfu ya watu walijiunga na maandamano ya mashoga jana huku wakibeba bendera za rangi tofauti na miavuli katika shinikizo la kutaka usawa , wiki kadhaa baada ya kiongozi wa nchi hiyo kusababisha malalamiko kwa kutangaza kuwa alitibiwa ushoga miaka kadhaa iliyopita. 

Wakati Ufilipino ina sifa ya kuwakubali mashoga na watu wa jinsia mbili, ndoa kati ya watu wa jinsia moja hazikubaliki na ulinzi wa sheria pia haupo. 

Rais Rodrigo Duterte mara kwa mara amekuwa akitumia maneno ya kebehi kwa mashoga dhidi ya wakosoaji na aliuambia mkusanyiko wa watu mwezi uliopita kwamba katika ujana wake, alijitibu dhidi ya ushoga kwa msaada wa wanawake warembo.

Talaka, utoaji mimba na ndoa za jinsia moja ni haramu katika taifa hilo linalozingatia zaidi imani ya kikatoliki ambapo muswada wa wa haki za mashoga haujapata ufanisi mkubwa katika sheria baada ya miongo kadhaa ya shinikizo.
Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAELFU WAANDAMANA KUTAFUTA USAWA KUHUSU USHOGA MAELFU WAANDAMANA KUTAFUTA USAWA KUHUSU USHOGA Reviewed by By News Reporter on 6/30/2019 06:59:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.