Loading...

SIRRO ASEMA NENO BAADA YA WATANZANIA 9 KUUAWA MSUMBIJI

Loading...
Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro amesema watanzania wapatao 9 wameuawa na wengine 6 kujeruhiwa nchini Msumbiji ambako walikwenda kujitafutia riziki.

Alivyoongea jana mkoani Mtwara eneo la mpaka wa Tanzania na Msumbiji alisema mauaji hayo yamefanyika Juni 26, 2019 ambapo pia watu wa Msumbuji kadhaa nao wameuawa.

''Waliofanya haya matukio tutawatafuta na nimeongea na IGP mwenzangu wa Msumbiji nimemuomba kukutana Juni 30, 2019 ili tuongee juu ya tukio hili na mengine'', amesema.

IGP Sirro alisema amesikitishwa sana na vifo vya watanzania hao ambao wamepigwa risasi na watatumia kila njia kuwapa waliofanya mauaji hayo.

Pia ametoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao pamoja na majeruhi 6 walionusurika kwenye mauaji hayo. Amewataka wananchi watoe taarifa zinazoweza kusaidia kupatikana kwa wauaji hao.

Imeelezwa kuwa watanzania hao huenda nchini Msumbiji wakati wa msimu wa kilimo kwaajili ya kulima na kujipatia mazao pamoja na kipato.
Na Yusufu Mashaka.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SIRRO ASEMA NENO BAADA YA WATANZANIA 9 KUUAWA MSUMBIJI SIRRO ASEMA NENO BAADA YA WATANZANIA 9 KUUAWA MSUMBIJI Reviewed by By News Reporter on 6/30/2019 07:25:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.