Loading...
Mwenyekiti wa Kamati ya Ushindi ya Stars na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliwasili jijini Cairo asubuhi ya jana tayari kwa kuongeza hamasa kuelekea mchezo wa leo wa Taifa Stars dhidi ya Kenya.
Makonda amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Misri Meja Jenerali Mohamed Nassoro pamoja na Rais wa TFF, Wallece Karia.
Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cairo, Makonda alisema bado anaamini Stars inaweza kufanya vizuri katika mechi zake mbili zilizosalia.
Makonda alisema kwa sasa mara baada ya kuwasili anataka kwanza kuonana na wachezaji kujua hali zao kabla ta mechi ya kesho.
Kiongozi huyo alisema shabiki kweli na mzalendo hawezi kukata tamaa baada ya Stars kupoteza mechi ya kwanza.
Alisema Stars ina wachezaji bora ambao bado wana nafasi ya kufanya vyema mbele ya Kenya iliyopoteza mechi ya kwanza pia.

Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAKONDA ATUA MISRI KUSHUHUDIA MECHI KATI YA STARS NA KENYA
Reviewed by By News Reporter
on
6/27/2019 09:10:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: