Loading...

MAREKANI YAANZA KUISHAMBULIA IRAN KWA MADAI YA KULIPA KISASI

Loading...
Marekani imeanzisha mashambulizi ya mtandao kwenye mifumo ya silaha za Iran siku ya Alhamisi wakati Rais wa Marekani Donald Trump alipoachana na mashambulizi ya anga, Ripoti nchini Marekani zimeeleza.

Mashambulizi hayo ya mtandaoni yameharibu mifumo ya kompyuta inayodhibiti roketi na mitambo ya kurushia makombora, limeeleza gazeti la Washington Post.

Tukio hilo ni kulipiza kisasi tukio la kushambuliwa kwa ndege yake isiyo na rubani pia mashambulizi dhidi ya meli za mafuta ambazo Iran imedaiwa na Marekani kuziteketeza,New York Times imeeleza.

Marekani pia imeweka vikwazo ambavyo rais Trump ameeleza kuwa ''vikubwa''. Na vikwazo hivyo ni kama; Ununuzi wa noti za Marekani unaofanywa na Iran, Biashara ya dhahabu na vyuma vingine, Graphite, aluminium, chuma, mkaa na programu zinazotumiwa katika sekta ya viwanda, Ubadilishanaji wa fedha unaohusishwa na sarafu ya Iran, Vitendo vinavyohusishwa na ulipaji madeni ya Iran na Sekta ya magari ya Iran

Amesema vikwazo vilikua vinahitajika kuizuia Iran kutengeneza silaha za nyukilia na vikwazo vya kiuchumi vitaendelea mpaka pale Tehran itakapobadili uelekeo.

Mvutano kati ya Marekani na Iran ulijitokeza tangu Marekani ilipojiondoa kwenye mkataba wa nyukilia wa mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani na kuiwekea vikwazo vilivyotikisa uchumi wa Iran.

Juma lililopita, Iran ilisema itaongeza viwango vilivyowekwa kwenye mkataba ule kuhusu mradi wa nyukilia.

Trump alisema hataki vita na Iran, lakini alionya kuwa Iran itakabiliwa na ''uharibifu'' ikiwa mzozo utatokea.
Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAREKANI YAANZA KUISHAMBULIA IRAN KWA MADAI YA KULIPA KISASI MAREKANI YAANZA KUISHAMBULIA IRAN KWA MADAI YA KULIPA KISASI Reviewed by By News Reporter on 6/24/2019 06:14:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.