Loading...
Mwanamke mmoja raia wa DR Congo amekuwa mgonjwa wa pili kufariki Uganda kwa ugonjwa wa Ebola tangu kutangazwa rasmi kuwa ugonjwa huo umevamia nchini humo, Wizara ya Afya ilitaarifu jana Alhamisi.
Mwanamke huyo ni bibi wa mtoto aliyefariki Alhamisi jioni baada ya kuingia Uganda kwenda kuwatembelea ndugu zake akitokea nchi jirani ya DR Congo.
"Bibi nae alifariki usiku wa jana," Afisa, Emmanuel Ainebyona, aliiambia mtandao wa habari wa Reuters.
Ainebyona alisema wagonjwa wengine wawili wapo katika uchunguzi na matibabu zaidi - mdogo wa kijana aliyefariki na kijana wa miaka 23 wa Uganda ambao wameonyesha dalili za ugonjwa huo wa Ebola.
Watu 27 zaidi wanafuatiliwa kwa ukaribu kwa vipimo ili kuhakikisha wanamaliza ugonjwa huo.
Ugonjwa huu wa Ebola kwa sasa ulianza kulipuka kuanzia DR Congo Agosti mwaka jana mashashariki mwa Congo na walishaambukizwa watu 2,062 , na kuua watu 1,390 kati yao. Na kwa mara ya kwanza umeingia Uganda ukitokea nchini DR Congo.

Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MGONJWA WA PILI AFARIKI KWA EBOLA UGANDA
Reviewed by By News Reporter
on
6/14/2019 10:09:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: