Loading...

WAKENYA WAWATIMUA WACHINA KWA UBINAFSI KATIKA BIASHARA

Loading...
Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i amewatimua nchini humo wafanyabiashara saba wa Kichina waliopatikana na hatia ya kufanya biashara zao kinyume cha sheria katika soko la maarufu kwa mitumba -Gikomba.

Hii ni baada ya Wakenya wanaouza bidhaa zao kwenye soko hilo lililopo jijini Nairobi kulalamikia ongezeko la Wafanyabiashara wa Kichina ambao walidai kuwa wanawaajiri wenzao na kuleta ushindani wa biashara.

Gikomba ni soko kubwa zaidi la nguo kuukuu au mitumba nchini Kenya.

Jumatano wiki hii Waziri wa mambo ya ndani alikuwa ameahidi kuwatimua wafanyabiashara wa kichina na wengine wa kigeni ambao watabainika kufanya biashara ndogo ndogo jijini Nairobi baada ya wakazi wa jiji hilo kulalamika kuwa Wachina wameleta ushindani mkubwa na wenyeji wanaofanya biashara katika masoko yanayouza nguo kuu kuu na bidhaa nyingine za bei za chini jijini humo ya Gikomba, Kamukunji na Nyamakima.

Wafanyabiashara katika soko maarufu la mitumba la Gikomba wanalalamika kuwa Wachina wanawaajiri Wachina wenzao kufanya kazi kama vile kupokea pesa na kuweka rekodi za mauzo, kazi ambazo hata Wakenya wanaweza kuzifanya, huku wakiwakodisha Wakenya kubeba mizigo kwa mikokoteni.

Kwa kiasi kikubwa Wachina katika soko la Gikomba huuza nguo za mitumba, mazulia, na viatu kutoka Uchina.

Katika masoko mengine ya Nyamakima na Kamukunji, Wachina huuza bidhaa za jumla kama vile nyaya za umeme, bidhaa za nyumbani, wanasesere na bidhaa nyingine ndogo ndogo za bei nafuu.
Na Haika Gabriel.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WAKENYA WAWATIMUA WACHINA KWA UBINAFSI KATIKA BIASHARA WAKENYA WAWATIMUA WACHINA KWA UBINAFSI KATIKA BIASHARA Reviewed by By News Reporter on 6/14/2019 10:12:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.