Loading...
Wizara ya Usalama wa ndani nchini Tunisia inasema afisa mmoja wa polisi amefariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya mripuaji wa kujitoa mhanga kulenga msafara wa polisi waliokuwa wanapiga doria katika mtaa wenye shughuli nyingi za kibiashara katikati mwa mji mkuu Tunis.
Shambulizi hilo limefanyika kwa kufuatana na shambulizi jengine katika makao makuu ya serikali ya kukabiliana na ugaidi viungani mwa mji wa Tunis.
Karibu watu wanane wengine wamejeruhiwa tayari wakiwemo maafisa watano wa polisi. Kulingana na walioshuhudia mripuko huo wa pili umefanyika baada ya mripuaji wa kujitoa mhanga kujaribu kuvamia jengo hilo la serikali lakini akazuiliwa na maafisa wa polisi.
Tunisia imeshuhudia msururu wa mashambulizi ya wanamgambo huku kundi linalojiita Dola la Kiislamu likidai kuhusika na mashambulizi hayo.

Na Zaida Msafiri.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MMOJA AFARIKI HUKU WENGINE WANANE WAJERUHIWA KATIKA SHAMBULIZI LA KIGAIDI TUNISIA
Reviewed by By News Reporter
on
6/28/2019 08:21:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: