Loading...
Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 38 amekamatwa na maafisa wa polisi wa Uhispania baada ya kunaswa na kilogram 29 za dawa za kulevya aina ya Cocaine ndani ya ndege ya Rais wa Brazil.
Dawa hizo zilipatikana ndani ya mizigo ya abiria mmoja wakati ndege hiyo ilitua katika uwanja wa ndege wa Seville kufanyiwa ukaguzi.
Imeripotiwa kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea Osaka nchini Japana ambapo Rais wa Brazili alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa G-20.
Mshukiwa ambaye alidaiwa kusafiri na marais 3 wa nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 29 alizuiliwa katika jela moja nchini Uhispania huku uchunguzi dhidi yake ukianzishwa.
"Wizara ya ulinzi iliripoti kuwa afisa mmoja anayeaminika kuwa wa jeshi la anga alishukiwa kwa kusafirisha dawa za kulevya ndani ya ndege ya Rais na amezuiliwa katika uwanja wa ndege wa Seville nchini Uhisoania,"Taarifa ya wizara ya ulinzi Uhispania iliripoti.

Na Haika Gabriel.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JAMAA ANASWA AKISAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA KWENYE NDEGE YA RAIS WA BRAZIL
Reviewed by By News Reporter
on
6/28/2019 07:51:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: