Loading...
Maafisa wa polisi wanaotaka kujiunga na kikosi kipya cha ulinzi wa taifa nchini Mexico wamepewa hadi miezi sita kupunguza uzani la sivyo wafutwe kazi.
Maafisa hao wamepewa agizo hilo wanapoendelea na shughuli ya kukabiliana na wahamiaji haramu.
Maafisa 625 tayari wamefeli vigezo vya kiafya vya kujiunga na kikosi hicho kitakacho hudumu katika mpaka wa Kaskazini na Kusini mwa nchi hiyo kwa miezi sita au zaidi, lilisema gazeti la El Financiero katika ripoti yake.
Maafisa ambao hawatafikia vigezo hivyo watalazimika kusalia katika katia vitengo vingine vya ulinzi wa taifa lakini pia wanakabiliwa na tisho la kufutwa kazi kwasababu kuna mpango wa kuunganisha idara ya polisi na vitengo vingine vya ulinzi kufikia mwisho wa mwezi Juni.
Taarifa hiyo ilifichuka baada ya kanda ya rekodi yenye sauti ya kamanda wa polisi Raúl Ávila Ibarra, iliyovujishwa kupatikana na gazeti la El Universal,.
Katika kanda hiyo afisaa huyo wa ngazi ya juu anasikika akijaribu kuwashawishi maafisa wadogo kujiunga na na kitengo kipya cha huduma ya uhamiaji huku akiwaelezea kuwa kitengo hicho kipya kinalipa vizuri kuliko chao polisi ".
"Wengine wetu tulio na uzani mkubwa tuna hadi miezi sita kubuni mbinu ya kufukia masharti tuliyopewa," Bw. Ávila Ibarra alisikika akisema.
El Financiero linasema kuwa maafisa wanaotoa maombi yakazi wa kitengo kipya cha ulinzi wa taifa hawatakiwi kuwa na uzani jumla wa mwili unatakiwa kuwa na BMI ya chini ya 28, hakuna kutopoa sehemu yoyote ya miwili wala kuwa na tattoos ambayo itaonekana watakapovalia sare za kazi.
Uchunguzi uliofanywa na shirika la kitaifa la takwimu na Geografia mwaka 2017 ilibaini kuwa 79 ya maafisa wa polisi walikuwa na uzani mkubwa kupita kiasi ilisema ripoti ya gazeti la Mexico News.

Na Yohana Zella.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
POLISI 'VIBONGE' KUFUTWA KAZI NCHINI MEXICO
Reviewed by By News Reporter
on
6/28/2019 07:25:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: