Loading...

RAIS MAGUFULI AZIDI KUNG'AA KIMATAIFA, JARIDA LA FORBES LAMTABIRIA MAKUBWA

Loading...
RAIS John Magufuli, ameendelea kukubalika kimataifa baada ya jarida maarufu duniani la Forbes kubashiri kwamba ataivusha Tanzania na kuwa nchi yenye kipato cha kati kupitia ajenda yake ya Tanzania ya viwanda chini ya mpango wa maendeleo wa 2025.

Jarida hilo la Forbes Afrika la Julai mwaka huu, ambalo lilikuwa mahsusi kwa ajili ya kelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano na uongozi wa Rais Magufuli, imeelezwa maono yake kama kiongozi wa nchi yameifanya Tanzania kupiga hatua kubwa za maendeleo na inatarajiwa kuwa miongoni mwa nchi chache sana za Afrika zenye maendeleo yanayoonekana na yanayopatikana kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa jarida hilo ambalo limemwelezea Rais Magufuli kama ‘Tingatinga’ katika kusimamia kile anachokiamini, miongoni mwa mambo makubwa yanayomfanya ang’ae kimataifa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge (SGR), upanuzi wa bandari na ujenzi wa miundombinu ya barabara zinazounganisha nchi nzima ambazo ni kichocheo kikubwa cha maendeleo hapa nchini.

Aidha, Rais Magufuli, ameelezewa kuwa ni mtu asiye na masihara katika kusimamia masuala ya maendeleo, mfano jinsi alivyosimamia na kuhakikisha Uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere (JNIA), terminal three, unakamilika kwa wakati na kwa kiwango cha kimataifa.

Jarida la Forbes limeendelea kumwelezea Rais Magufuli kuwa, mafanikio mengi anayopata ni kutokana na kuongozwa na mpango wa maendeleo wa 2025 pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015.

Mahojiano ya Rais Magufuli yaliyotolewa na Jarida la Forbes Africa, yalifanyika mapema mwaka huu na jarida hilo lilikuwa na toleo maalum la Tanzania kuhusiana na mambo mbalimbali yanayotekelezwa na serikali.
Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIS MAGUFULI AZIDI KUNG'AA KIMATAIFA, JARIDA LA FORBES LAMTABIRIA MAKUBWA RAIS MAGUFULI AZIDI KUNG'AA KIMATAIFA, JARIDA LA FORBES LAMTABIRIA MAKUBWA Reviewed by GEOFREY MASHEL on 6/21/2019 07:21:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.