Loading...

SERIKALI YA MISRI YAKATAZA KUFANYIKA MAADHIMISHO YA MSIBA WA MORSI

Loading...
Mtoto wa kiume wa Rais wa Misri aliyefariki mahakamani Muhammed Morsi amesema mamlaka nchini humo zilizuia kufanyika maadhimisho stahiki kwa ajili ya msiba wa baba yake

Abdullah Morsi mtoto wa Muhammed Morsi, Rais wa kwanza  wa Misri na pekee aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia ambaye alipoteza maisha akiwa mahakamani, amesema mamalaka nchini Misri ziliwakataza kufanya maadhimisho ya msiba wa baba yake.

Katika maelezo aliyoyatoa kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii Abdullah Morsi alisema mamlaka nchini Misri zimezuia yasifanyike maadhimisho stahiki ya msiba, kwa ajili ya baba yake ambaye alikuwa ndio Rais wa kwanza wa kihistoria kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.

Morsi aliongeza kwamba hata kupokea salamu za rambi rambi katika nyumba ya baba yake wamekatazwa.

Abdullah Morsi alisema kwamba pamoja na vikwazo hivyo vilivyowekwa na mamlaka nchini Misri, Kitendo cha maeneo mbalimbali duniani kumswalia swala ya “ghaib” kilimtia faraja.

Mamlaka nchini Misri hazijasema chochote kuhusiana na mada hio. Siku ya Jumatatu Muhammed Morsi alifariki dunia akiwa mahakamani kujibu mashitaka ya ujasusi.
Na Lucky Richard.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SERIKALI YA MISRI YAKATAZA KUFANYIKA MAADHIMISHO YA MSIBA WA MORSI SERIKALI YA MISRI YAKATAZA KUFANYIKA MAADHIMISHO YA MSIBA WA MORSI Reviewed by By News Reporter on 6/20/2019 07:33:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.