Loading...
Mnamo mwezi Machi, 2019 serikali ilitangaza kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya Dengue ambao hauna dawa mara baada ya watu 11 kuambukizwa na kulazwa jijini Dar es salaam.
Ugonjwa huo umezidi kushamiri kwani kwa mujibu wa taarifa za serikali watu wanne wamepoteza maisha nchini humo kwa sababu ya homa ya Dengue na wengine 4,000 wameambukizwa na wanaendelea kupata matibabu.
Waziri wa afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amewaambia wabunge jijini Dododma siku ya Ijumaa kuwa, watu watatu wamepoteza maisha jijini Dar es salaam na mwingine mmoja jijini Dodoma.
Aidha, ameeleza kuwa vifo vya watu wawili, vilitokea mwezi Mei.
Waziri Mwalimu, ameongeza kuwa serikali imeweka mikakati ya kupambana na homa hiyo na kuagiza kuwa vipimo vya Dengue katika hospitali za umma, viwe bure.
Homa ya Dengue huenezwa kwa kupitia kuumwa na mbu anayebeba virusi wa ugonjwa huo.

Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UGONJWA WA DENGUE NA HALI ILIVYO, WALIOAMBUKIZWA WAFIKIA 4000
Reviewed by By News Reporter
on
6/24/2019 06:45:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: