Loading...
KUNA mengi yanayoiunganisha dunia kupaza sauti moja katika dhima nzima ya kupigania maendeleo ya binadamu kwenye zama hizi, ilhali haki za makundi tofauti na zaidi yaliyo pembezoni zinapewa kipaumbele.
Miongoni mwa makundi yaliyo pembezoni kwa mujibu ya Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2016 iliyotolewa na Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) ni ya wanawake na wasichana.
Makundi hayo yanakabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwemo janga la ukeketaji ambalo limepigiwa kelele na linaendelea kupigiwa kelele na dunia hadi sasa ili litokomezwe.
Sasa pamoja na juhudi kubwa za kutokomeza janga hili kuchukuliwa kwenye uga wa kimataifa katika sekta mbalimbali ni kwa nini unaendelea kutendeka, ni swali ambalo wengi wanajiuliza.
Hata hivyo, baadhi ya sababu kubwa zinazotajwa kuwa chanzo cha kuendelea kushamiri kwa ukeketaji hata katika zama hizi za utandawazi ni kukubalika katika jamii, dini, imani potofu juu ya usafi wa mwili na kuhifadhi ubikira.
Na kubwa zaidi kwenye makabila na jamii zinazoendeleza mila hii ni kumwezesha mwanamke aolewe.
Kwamba ameshaingia katika utu uzima na anafaa kuwa mke wa mtu mwenye heshima kimila.
MBINU MPYA ZINAZOTUMIKA KUKWAMISHA JUHUDI ZA KUTOKOMEZA JANGA HILI
Kabila la Wakurya lililoko katika mkoa wa Mara, linatajwa kuendeleza ukeketaji likitumia mbinu mpya za kificho. Kwa mfano: Jamii ya Kikurya inapoona imebanwa kwa upande wa Tanzania, hukimbilia kutekeleza mila hiyo upande wa Kenya.
Kabila hilo linatajwa kuendeleza mila hiyo kwa imani kuwa binti ambaye hajakeketwa katika jamii anahesabika ni laana na mkosi kwa ukoo wake.

Na Ummy Kitwana.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WAKURYA NA MBINU MPYA ZA UKEKETAJI
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
6/19/2019 08:36:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: