Loading...
Viongozi wa klabu ya Man United, wanaripotiwa kuanzisha mchakato wa kumtafuta mrithi wa Paul Pogba baada ya Mfaransa huyo kutangaza nia yake ya kuondoka katika klabu hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti za The Mirror, kuondoka kwa Pogba uwanjani Old Trafford, msimu huu wa kiangazi, utaweka United katika athari kubwa sehemu ya ushambuliani, huku kiungo huyo akiwa na hamu kubwa ya kujiunga na Real Madrid msimu ujao.
Meneja wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer, yuko mbioni kunoa makali ya kikosi chake kwa kutafuta huduma za Daniel James wa Swansea City, na viungo wengine wa kati kama vile Adrien Rabiot, Youri Tielemans na Bruno Fernandes.
Taarifa zingine kutoka kwa gazeti la spoti nchini Uhispania, zinaripoti kuwa nyota wa PSG Neymar, pia analengwa na Man United baada ya matamshi yaliyotolewa na rais wa klabu hiyo Nasser Al Khelaifi.
Licha ya kutomtaja staa huyo raia wa Brazil, kwenye matamshi yake, Nasser alionekana kumlenga Neymar wakati akizungumzia kuhusu kikosi chake.
"Wachezaji wanapaswa kurejelea majukumu yao. Mambo yanapaswa kuwa tofauti wanatakiwa kujituma zaidi. Hawapo hapa kufanya mchezo na kama hawakubaliani nami basi waondoke. Sitaki tabia za kupotoshwa na ustaa," alisema Al Khelaifi katika mahojiano na France na football.

Na Aziza Omari.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
NEYMAR KUMRITHI POGBA MAN UTD?
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
6/19/2019 08:03:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: