Loading...

ZIJUE DALILI NA MAMBO YANAYOSABABISHA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO

Loading...
VIDONDA VYA TUMBO NI NINI?
Vidonda vya tumbo (Peptic Ulcers) ni ugonjwa unaompata mtu ambapo kunatokea vijitundu au michubuko katika kuta za ndani za viungo vya mfumo wa uyeyushaji chakula. Michubuko hiyo huweza kutokea katika eneo la mfuko wa tumbo, katika duodenum au katika eneo la koo. Inakadiriwa kuwa asilimia 5 hadi 10 ya watu hupatwa na ugonjwa huu angalau mara moja katika maisha yao. 

Huu ni ugonjwa ambao unaweza kumrudia mtu baada ya kupona endapo chanzo chake hakikudhibitiwa. Kama ugonjwa huu utamrudia mgonjwa , mtu huyu atakuwa amejiweka kwenye hatari kubwa ya kupata madhara makubwa zaidi kama kutokwa na damu au kutokea tundu kubwa katika kuta za mfuko wa tumbo.

DALILI ZA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO:
- Kuchoka choka sana bila sababu maalum
- Kuuma mgongo au kiuno
- Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia
- Kizunguzungu
- Kukosa usingizi
- Usingizi wa mara kwa mara
- Maumivu makali sehemu ya mwili
- Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali. Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali
- Kichefuchefu
- Kiungulia
- Tumbo kujaa gesi
- Tumbo kuwaka moto
- Maumivu makali sehemu kilipo kidonda
- Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi
- Kutapika nyongo
- Kutapika damu au kuharisha
- Sehemu za mwili kupata ganzi
- Kukosa hamu ya kula
- Kula kupita kiasi
- Kusahahu sahau na
- Hasira bila sababu.

VITU VINAVYOHUSIKA KULETA VIDONDA VYA TUMBO MWILINI:

a). Asidi iliyozidi mwilini:
Unapokaribia kutaka kula chakula chochote, au ukiwaza kutaka kula au ukiuona tu msosi kwa macho, tumboni mwako huzalishwa haidrokloriki asidi ili kuuandaa na kuusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Kadri unavyoendelea kuishi haidrokloriki Asidi hiyo huenda kutoboa kuta za tumbo ndani na hatimaye taratibu baadaye hukusababishia VIdonda vya tumbo.

b). Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha:
Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha ni moja ya vipengele vikuu vinavyosababisha vidonda vya tumbo.Mfadhaiko huongeza utiririkaji wa asidi ndani ya tumbo. Hii asidi ya ziada ambayo hutiririka ndani ya tumbo kama matokeo ya mfadhaiko na hakuna chakula cha kufanyiwa kazi au kumeng’enywa humomonyoa kuta za tumbo na hivyo kusababisha vidonda.

Kwahiyo ili kuepuka ugonjwa huo, usiruhusu hapo juu kutokea.
Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
ZIJUE DALILI NA MAMBO YANAYOSABABISHA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO ZIJUE DALILI NA MAMBO YANAYOSABABISHA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO Reviewed by By News Reporter on 6/29/2019 06:37:00 AM Rating: 5

Maoni 1 :

  1. Mtu akiambiwa kuwa tumbo lake limejaa maji na anavidonda kwenye ini kunauwezekano wa kupona

    JibuFuta

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.