Loading...
Ni kawaida kwa wapendwa wetu walioaga dunia kufanyiwa mazishi kisha kuzikwa ama kuchomwa kwa heshima.
Lakini nchini Marekani jimbo la Texas, mwanamke mmoja amekamatwa baada ya mabaki ya mwili wa mama yake yaliyooza kugunduliwa katika nyumba wanakoishi pamoja na mjukuu wa marehemu.
Polisi wanaamini mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 71 alianguka na hatimaye kuaga dunia mnamo 2016.
Kulingana na ripoti ya shirika la BBC, polisi wanamtuhumu binti ya marehemu mwenye umri wa miaka 47 alishindwa kumtunza vyema mama yake aliyefariki siku chache baadaye kutokana majeraha aliyoyapata baadaya ya kuanguka.
Mabaki ya mwili wa marehemu yalipatikana kwenye sakafu ya chumba kimoja tofauti na walicholala binti yake na mjukuu.
Ripoti hiyo ambayo Dundiika News imeisoma inaendelea kusema kuwa, mjukuu wa marehemu ana umri wa miaka 15 na kutokana na hilo, mamake ameshtakiwa kwa kosa la kumdhuru mtoto wa chini ya miaka 15.
Mjukuu huyo sasa anaishi na jamaa zao na anapokea usaidizi kutoka kitengo cha kuwalinda watoto.
Akipatikana na hatia, mama yake huenda akakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 20 gerezani na faini ya hadi $10,000 ambazo ni sawa na TSh 23 milioni.
Polisi wanasema marehemu aliheshimika katika jamii katika eneo hilo, na alifanya kazi ya ukarani licha ya kuwa mwalimu msaidizi katika mojawapo wa shule katika eneo hilo kwa miaka 35.
Alipostaafu, alikuwa akifanya kazi ya kukusanya tiketi katika sherehe za michezo huko Seguin.

Na Zaida Msafiri.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
ALIYEKUWA AKIISHI NA MAITI MIAKA 3 ASWEKWA NDANI
Reviewed by By News Reporter
on
7/15/2019 05:44:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: