Loading...
Wakenya wamefurahishwa na baadhi ya viongozi waliohudhuria harusi ya gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru Mumbi na wakili Kamotho.
Viongozi hao wakiwemo Rais Uhuru Kenyatta, kiongozi wa upinzani Raila Odinga na kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka walionekana wakisakata densi vilivyo na imekuwa gumzo mitandaoni.
Wakiongozwa na Uhuru, viongozi hao walionyesha umahiri wao katika kusakata dansi huku nyimbo za kitamaduni zikichezwa.
Hata hivyo, baadhi ya Wakenya walikuwa makini kutambua kuwa Raila hakuwa akicheza muziki sawa na mdundo wa nyimbo zilizokuwa zikichezwa.
"Subalkheri, nilidhani ni mimi pekee ndiye nisiyejua kusakata dansi ila hadi nilipomuona Raila akiparanganyika akiwa kwenye sherehe ya harusi ya Waiguri," Mkenya mmoja aliandika Twitter.
Aidha, Raila hakuwa kiongozi pekee asiyejua kusakata densi kwani naibu gavana wa Kirinyaga, Peter Ndambiri pia alionekana kuchanganya sana.

Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KENYATTA, RAILA WALIVYOSISIMUA MTANDAO KWA KUSAKATA RUMBA KWENYE HARUSI YA MWANASIASA MAARUFU KENYA
Reviewed by By News Reporter
on
7/15/2019 05:31:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: