Loading...
Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO limeutambua mji wa kale wa Babylon kuwa eneo la kihistoria.
Iraq imekuwa ikishinikiza tangu mwaka 1983 mji huo wa kale wa miaka 4,000-uijumuishwe katika orodha ya kifahari ya Umoja wa Mataifa.
Mji huo ulijulikana kwa bustani zake za kuning'inia, ambazo zilikuwa kati ya Maajabu Saba ya Dunia ya vitu vya kale duniani.
Miaka ya hivi karibuni eneo hilo limeharibiwa kufuatia ujenzi wa kasri la Saddam Hussein, na baadae kutumiwa kama kambi ya kijeshi kwa vikosi vya Marekani.
Kamati ya Urithi wa Dunia ya Umoja wa Mataifa ilikutana nchini Azerbaijan kuamua kuhusu maeneo mapya ya kale ambayo yanastahili kutambuliwa - ili yapewe tuzo kwa kuwa maeneo au nembo ya kihistoria inayozingatia muhimu binadamu wote na kulindwa na mikataba ya kimataifa.
Ujumbe wa Iraq ulikaribisha hatua hiyo, ukisema kuwa huu ni utambuzi wa mchango wa Babylon katika ustaarabu wa Mesopotamia.
Ikitangaza uamuzi huo, Unesco ilisema: "Hatua hii inaashiria utambuzi wa ubunifu wa hali ya juu ya mji wa-Babylon.
"Kuhusishwa kwa mji huo na moja ya maajabu saba ya vitu vya kale duniani.
Pia ilionya kuwa maeneo hayo yako katika "hali mbaya" na kwamba yanahitaji kuhifadhiwa haraka iwezekanavyo.

Na Fatma Omari.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
BABYLON YATAMBULIWA KAMA MJI WA KIHISTORIA KWA MAAJABU YAKE
Reviewed by By News Reporter
on
7/06/2019 06:06:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: