Loading...

'KUMBE KUTUKANA KUNAONGEZA AFYA?'

Loading...
Pengine sote tumewahi kutukana katika maisha yetu.

Ama ni kutokana na hasira au kwa sababau yoyote ile nyingine, lakini ni sehemu nzito ya lugha inayotumika na watu katika makabila tofuati.

Nchini Ukraine, kaimu waziri wa afya Ulana Suprun amependekeza kwamba matusi ni mazuri kwa afya yako kutokana na kwamba mtu anapotusi, inaashiria uhusiano mzito ulioimarika na ni 'mawasiliano mazuri ya kihisia' baina ya watu.

Suprun alikuwa anazungumzia sheria iliyopendekezwa ya kusitisha lugha chafu katika vyombo vya habari.

Sheria hiyo inaeleza kwamba watu wanaotukana hewani na katika hotuba kwa umma, watatozwa faini ya hadi $49.

Lakini mtazamoa wa Dkt Suprun ni kwamba kutukana au matusi ni muhimu katika hali mbaya akisema "katika visa kadhaa matusi humaanisha watu wana ukaribu na kwamba kuna mawasiliano mazuri ya kihisia kati yao".
Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
'KUMBE KUTUKANA KUNAONGEZA AFYA?' 'KUMBE KUTUKANA KUNAONGEZA AFYA?' Reviewed by By News Reporter on 7/07/2019 06:51:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.