Loading...

DIAMOND PLATINUMZ AWA BALOZI WA UKIMWI KUPITIA TACAIDS

Loading...
Ni siku tatu baada ya mengi kuzungumzwa kuhusu sherehe ya kuzaliwa ya mama yake mzazi na mama wa mtoto wake mtarajiwa, Tanasha Donna. Nyota wa Bongo Fleva Diamond Platinumz amechaguliwa kuwa balozi wa TacAids.

Tume ya kukabiliana na janga la UKIMWI nchini Tanzania TACAIDS ilitangaza Jumatano Julai 10 jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa tume hiyo na msanii huyo wa lebo ya Wasafi Records

Kaimu mkurugenzi wa Tume hiyo Jummanne Issango alisema wakati wa mkakati wa nne wa kuangamiza Ukimwi kwamba tume hiyo inawahamasisha vijana kuhusu afya ya uzazi pamoja na kutoa hamasa kuhusu ugonjwa huo.

Akizungumza baada ya uteuzi wake Diamond Platinumz alisema kwamba iwapo wanawake wangekataa katakata kuwaruhusu wanaume kushiriki tendo la ngono bila kinga basi hatua hiyo ingepunguza maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi nchini humo.

Kulingana na mtandao huo, Diamond alikuwa akijibu swali kutoka kwa mwandishi aliyetaka kujua ni vipi msanii huyo atafanya kampeni hiyo kupitia tamasha linalokuja la Wasafi na jinsi yeye mwenyewe alivyomwaminifu kwa wapenzi wake.

''Ninaamini kwamba iwapo wanawake watatilia mkazo swala la hakuna ngono bila kinga wanaume watalazimika kutumia kinga''.

Akizungumzia kuhusu ushirikiano wa kufanya kazi na TACAIDS kupitia tamasha la Wasafi, alisema kuwa kampeni hiyo imejiri wakati mzuri kwa kuwa tamasha hilo sio tu kuhusu burudani bali pia kutoa elimu kwa vijana.

Afisa wa baraza la sanaa nchini Tanzania Basata aliunga mkono hatua hiyo ya TACAIDS akisema kuwa walifanya uamuzi mzuri kuwatumia wasanii kutokana na ushawishi walio nao miongoni mwa Vijana kupitia mitandao ya kijamii.

Tamasha hilo la Wasafi linatarajiwa kuanza Julai 19 2019.
Na Vicky Shadrack.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
DIAMOND PLATINUMZ AWA BALOZI WA UKIMWI KUPITIA TACAIDS DIAMOND PLATINUMZ AWA BALOZI WA UKIMWI KUPITIA TACAIDS Reviewed by By News Reporter on 7/11/2019 06:45:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.