Loading...

FACEBOOK MATATANI, YAPIGWA FAINI KUBWA

Loading...
Tume ya udhibiti wa masuala ya kibiashara nchini Marekani imeidhinisha faini ya dola bilioni 5 dhidi ya kampuni ya mtandao wa habari wa Facebook kwa ajili ya uchunguzi wa udukuzi wa data binafsi, vinasema vyombo vya habari vya Marekani.

Tume hiyo (FTC) imekuwa ikifanya uchunguzi juu ya madai kwamba taasisi ya ushauri wa kisiasa ya Cambridge Analytica ilipata taarifa kwa njia isiyotakiwa za watumiaji milioni 87 wa mtandao wa Facebook.

Malipo hayo yaliiidhinishwa na tume ya FTC kwa kura 3-2, duru zimevihahamisha vyombo vya habari vya Marekani.

Facebook na FTC wameiambia BBC kiuwa hawana la kuzungumzia juu ya repoti hiyo ya uchunguzi.

Tume inayolinda maslahi ya watumiaji mtandao huo FTC ilianza kuichunguza Facebook mwezi Machi 2018 kufuatia ripoti kwamba Cambridge Analytica iliweza kuzifikia taarifa/data za mamilioni ya watumiaji wa mtandao huo wa kijamii.

Uchunguzi huo ulijikita juu ya ikiwa Facebook ilikiuka makubaliano ya mwaka 2011 ambayo kwa mujibu wake ingepaswa kuwafahamisha wazi watumiaji wa mtandao huo na pia ''kuelezea hofu " ya kushirikishadata zao..

Gazeti la New York Times limeripoti kuwa chama cha Democrats kilitaka masharti makali yawekwe dhidi ya Facebook, huku baadhi ya wafuasi wa Democrats wakikosoa kuwa kiwango hicho cha faini hakifai.

Facebook imekuwa ikitarajia hatua hii dhidi yake. Iliwaeleza wachunguzi mwezi Aprili kuwa imetenga kando pesa nyingi kwa ajili ya sakata hiyo , kwa hiyo inamaanisha kuwa kampuni haijtateteleka kifedha kutokana na adhabu iliyopewa.

Kile kisichofahamika ni hatua gani zaidi zitakazochukuliwa au masharti zaidi itakayopewa Facebook, kama vile kuweka mikakati zaidi ya kulinda taarifa za kibinafsi au ikiwa kutakuwa na athari nyingine zai kwa Mkuu wake, Mark Zuckerberg.

Malipo hayo, ambayo ni karibu theluthi moja ya faida nzima ya kampuni, yanaweza kuchochea ukosoiaji kwa wale wanaoweza kusema kuwa kiasi hicho cha fedha ni kidogo
Na Lameck Daudi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
FACEBOOK MATATANI, YAPIGWA FAINI KUBWA FACEBOOK MATATANI, YAPIGWA FAINI KUBWA Reviewed by By News Reporter on 7/14/2019 09:39:00 AM Rating: 5

Maoni 1 :

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.