Loading...

MCHUNGAJI ADAIWA KUTEKWA BAADA YA KUMUITA RAIS MUSEVENI MWIZI, MUONGO

Loading...
Visa vya utekaji nyara vinaendelea kuripotiwa nchini Uganda na sasa watu wasiojulikana wanadaiwa kumteka nyara Mchungaji Joseph Kabuleta katika eneo la Forest Mall.

Ripoti kutoka nchini humo Ijumaa, Julai 12 zilisema, mwanahabari huyo wa zamani wa michezo alichukuliwa kutoka mgahawa mmoja katika jumba hilo na kutupwa ndani ya gari kabla ya gari hilo kuondoka.

Gazeti la Obsever lilisema kuwa, Kabuleta katika siku za karibuni amekuwa akiikashifu sana familia ya Rais Yoweri Museveni hasa baada ya rais kuweka mikakati ya kumpokeza mamlaka ya urithi wa urais mwanawe Jenerali Muhoozi Kainerugaba. 

Kufikia Ijumaa jioni hamna ripoti kamili zilizokuwa zimetolewa kuhusu aliko mchungaji huyo lakini sasa ripoti zinasema ni maafisa wa polisi waliomtia mbaroni.

Polisi walisema kupitia taarifa yao kuwa, Kabuleta yupo mikononi mwao na kulingana nao, Kabuleta mara kadhaa kupitia ukurasa wake wa Facebook amekuwa akimuita Museveni mcheza kamari, mwizi na muongo. 

Kabuleta ambaye ni mchungaji wa Kanisa la WatchMan Ministries, alitiwa mbaroni majira ya saa 11 jioni wakati akijitayarisha kwa maombi ya jioni.

Mchungaji huyo si wa kwanza kuripotiwa kutekwa nyara na watu ambao walikataa kujitambua lakini karibuni promota wa Bobi Wine Andrew Mukasa almaarufu Bajjo alichukuliwa na kutupwa ndani ya gari. Alitoweka siku kadhaa na baadaye kupatikana.
Na Geofrey Okechi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MCHUNGAJI ADAIWA KUTEKWA BAADA YA KUMUITA RAIS MUSEVENI MWIZI, MUONGO MCHUNGAJI ADAIWA KUTEKWA BAADA YA KUMUITA RAIS MUSEVENI MWIZI, MUONGO Reviewed by By News Reporter on 7/14/2019 09:24:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.