Loading...

MWANAHABARI MREMBO NA MAARUFU WA SOMALIA AUAWA KATIKA SHAMBULIZI LA KIGAIDI KISMAYU

Loading...
Mwanahabari wa Somali Hodan Nalayeh ambaye pia ni mwanzilishi wa Integrity TV ameuawa katika shambulizi lililotokea katika hoteli moja Kismayu ambalo pia lilimuua mume wake.

Nalayeh, 43, alikuwa ameishi mwaka mingi nchini Canada alikuwa amesafiri na familia yake kuja Somalia wakati kulipotokea uvamizi huo Ijumaa, Julai 12.

Mwanahabari huyo aliyekuwa mjamzito na mume wake Farid Jama waliuawa katika shambulio hilo.

Hadi kifo chake, Naleyah alikuwa ni mama ya watoto wawili na alifahamika sana kwa kueneza mila za jamii ya Somali miongoni mwa raia wa Canada na nia yake kutaka mabadilo pevu nchini mwao ilifahamika pakubwa. 

"Kupitia kazi yake ya uanahabari, alieleza habari nyingi muhimu sana kuhusu jamii yake na mchango wao nchini Canada na alikuwa sauti ya wengi," Waziri wa Somali wa Uhamiaji, Wakimbizi na Uraia Ahmed Hussein aliiambia CBC.

"Kazi yake, hasa katika kuwasaidia wanawake na vijana, aliimarisha uhusiano kati ya jamii ya Somali nchini Canada na Somalia unavyoendelea kukua kupitia udhabiti na ujengaji upya. Tunaomboleza kwa huzuni mwingi kifo chake, na wengine wote waliouawa kwenye shambulio la Kismayo," aliongezea. 

Familia na marafiki kutoka katika kona mbali mbali duniani, hasa Canada na Somalia, walimwomboleza Naleyah kuwa mwanamke ambaye mchango wake katika tasnia ya uanahabari unafaa kuigwa na wengi.
Na Frank Juma.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MWANAHABARI MREMBO NA MAARUFU WA SOMALIA AUAWA KATIKA SHAMBULIZI LA KIGAIDI KISMAYU MWANAHABARI MREMBO NA MAARUFU WA SOMALIA AUAWA KATIKA SHAMBULIZI LA KIGAIDI KISMAYU Reviewed by By News Reporter on 7/14/2019 09:12:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.