Loading...

FORBES: TAYLOR SWIFT NI STAA ANAYEONGOZA KUINGIZA PESA NYINGI DUNIANI

Loading...
Orodha mpya ya Forbes inasema mwanamuziki Taylor Swift ndiye aliyeongoza kuingiza pesa nyingi kwa mwaka 2018 mpaka sasa, kiasi kinakadiriwa sawa na dola za kimarekani milioni $185 (sawa na zaidi ya bilioni 430 pesa za Tanzania) kwa mujibu wa jarida hilo.

Akiongoza katika orodha ya mastaa 100 iliyotangazwa jana Jumatano Julai 10, imeelezwa kuwa kiasi cha makadirio ya pesa alizotengeneza kwa mwaka 2018 ni zaidi ya asilimia 131 ya kiasi chote alichotengeneza mwaka 2017, ambapo kilikuwa sawa na dola za kimarekani milioni $80. Mara ya mwisho alipokuwa kileleni ilikuwa mwaka 2016 alipoingiza kiasi cha dola za kimarekani milioni $170 zilizotokana na tamasha lake la '1989 World Tour'.

Aliyemfuatia ni Kylie Jenner, bilionea mtoto ambaye ameshikilia nafasi ya pili baada ya kuingiza kiasi cha dola za kimarekani milioni $170, Kanye West ni wa tatu kwa kuingiza kiasi cha dola za kimarekani milioni $150.
Na Frank Kavikule.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
FORBES: TAYLOR SWIFT NI STAA ANAYEONGOZA KUINGIZA PESA NYINGI DUNIANI FORBES: TAYLOR SWIFT NI STAA ANAYEONGOZA KUINGIZA PESA NYINGI DUNIANI Reviewed by By News Reporter on 7/11/2019 09:11:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.