Loading...
Viongozi wa vuguvugu linalounga mkono demokrasia nchini Sudan limekaribisha makubaliano yaliyofikiwa mapema ya jana ya kuundwa kwa serikali ya pamoja na baraza la mpito la kijeshi.
Wamesema ni ushindi wa mapinduzi waliyoyaanzisha, unaofufua pia matumaini ya kumalizika kwa mvutano wa miezi mitatu na baraza hilo, na kusababisha machafuko mabaya.
Kwenye taarifa yao mapema ya jana waliyoichapisha kwenye ukurasa wa Facebook wa Jumuiya ya Wataalamu nchini humo, wamesema leo, mapinduzi yao yameshinda na ushindi wao unang'ara.
Kulingana na taarifa ya jumuiya hiyo, pande hizo mbili zimekubaliana kuunda baraza tawala la pamoja kuongoza nchi hiyo katika kipindi cha mpito cha miaka mitatu na miezi mitatu.
Alipozungumza baada ya makubaliano hayo, kiongozi wa kundi la Forces of Declarartion of Freedom and Change, FDFC Omer al-Digair alisema"Makubaliano haya yanafungua njia ya kuunda utawala wa mpito utakaziba ombwe la kisiasa, uchumi na hata maisha ya kawaida. Suala litakalopewa kipaumbele na serikali hii ni kurejesha amani na uhuru, na uwazi katika uchunguzi wa wahusika wa mauaji ya mashahidi ili wawajibishwe"
Lakini pia, makamu wa rais wa baraza hilo la kijeshi Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo alisema, "Mkataba huu utakuwa mkamilifu, na hakutakuwa na uonevu dhidi ya mwingine lakini pia utatambua mahitaji ya watu wa Sudan pamoja na mapinduzi yao."

Na Ummy Kitwana.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
HATIMAYE SUDAN WAKUBALIANA, SERIKALI YA MPITO KUUNDWA
Reviewed by By News Reporter
on
7/06/2019 05:37:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: