Loading...

INDIA: MBUGE ALIYEMWAGIA NDOO YA MATOPE MUHANDISI KISA BARABARA MBOVU MBARONI

Loading...
Nchini India mbunge akasirishwa  kutokana na barabara kutokuwa na hali nzuri kitu kilichopelekea mbunge huyo kumwagia ndoo mbili za matope muhandisi wa barabara.

Mbunge huyo aliyefahamika kwa jina la Nitesh Rane alikerwa kutokana na barabara za Mumbai kutotunzwa vizuri akakusanya wafuasi wake na kwenda eneo ambalo kulikuwa kukifanyika ukarabati wa barabara.

Kwanza alimshambulia kwa maneno muhandisi aliyokuwa akisimamia ukarabati huo wa barabara na baadaye akamwogesha muhandisi huyo kwa ndoo mbili za matope. Tukio hilo lilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ndani ya muda mfupi na kuibua hisia mbalimbali.

Mbunge Nitesh Rane anashikiliwa na polisi.
Na Hamisi Jafari.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
INDIA: MBUGE ALIYEMWAGIA NDOO YA MATOPE MUHANDISI KISA BARABARA MBOVU MBARONI INDIA: MBUGE ALIYEMWAGIA NDOO YA MATOPE MUHANDISI KISA BARABARA MBOVU MBARONI Reviewed by By News Reporter on 7/06/2019 05:00:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.