Loading...

KOCHA MOURINHO AKATAA SHAVU CHINA

Loading...
Aliyekuwa Kocha wa Manchester United na Chelsea Jose Mourinho amekataa ofa ya kwenda kufundisha nchini China.

Mourinho amehusishwa na taarifa za kufuatwa na timu ya Guangzhou Evergrande akipewa ofa ya kitita cha pauni milioni 88.

Donge hilo lingemfanya kuwa kocha anayelipwa fedha nyingi duniani lakini Mourinho ametaka kuendelea kubaki Uingereza na familia yake.

Mourinho hajawa kazini tangu alipofukuzwa na Manchester United mwaka jana mwezi Disemba.

Guangzhou kwa sasa wanafundishwa na kocha muitaliano Fabio Cannavaro.

Mourinho alisema mwezi Machi kuwa anataka kurejea kwenye kazi yake ya ukocha mwaka huu, lakini anasubiri kazi itakayomfaa.

''Ninajua kwa hakika nisichokitaka,'' alisema.

''Ninajua ninachokitaka, si timu fulani lakini namna ya kazi ilivyo na ukubwa wa kazi.''
Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KOCHA MOURINHO AKATAA SHAVU CHINA KOCHA MOURINHO AKATAA SHAVU CHINA Reviewed by By News Reporter on 7/09/2019 08:01:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.