Loading...

MABASI YA MIKOA SASA KUSAFIRI HADI USIKU (SAA 24)

Loading...
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola amepiga marufuku Makamanda wa Polisi kuzuia mabasi yanayofanya safari kati ya Jiji la Dar es Salaam na Mikoa ya Kanda ya Ziwa kusafiri usiku kwa kisingizio cha kuhofia majambazi.

Waziri Lugola ametoa kauli hiyo Jumapili Julai 7, 2019 katika mkutano wa hadhara na wananchi wa vijiji vya Namibu na Mwibara wilayani Bunda mkoani Mara.

Pia Waziri Lugola, ametoa onyo kwa Makanisa na Misikiti nchini ambayo itashindwa kwenda kufanyiwa uhakiki itachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Akizungumzia swala la vitambulisho, Waziri Lugola, amesema anajua kuna kero ya kusajili simu kutokana na upatikanaji wa vitambulisho vya taifa, lakini kutokana na upungufu huo amewaelekeza Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kutoa namba ili waweze wananchi kuweza kuendelea na usajili na pia amewataka NIDA wampee takwimu za Wilaya zote ili kujua ukubwa wa tatizo la usajili wa vitambulisho hivyo.

Lugola ameongeza kuwa, hakuna mwananchi atakayekosa kitambulisho cha taifa, na NIDA itawafuata mahali popote walipo nchini.
Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MABASI YA MIKOA SASA KUSAFIRI HADI USIKU (SAA 24) MABASI YA MIKOA SASA KUSAFIRI HADI USIKU (SAA 24) Reviewed by By News Reporter on 7/08/2019 06:04:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.