Loading...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amaliza ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania na kurejea nchini mwake.
Katika ziara yake hiyo Kenyatta, amemjulia hali mama mzazi wa Rais Dkt. John Magufuli ambaye anaendelea na matibabu nyumbani kwake Chato, Geita.
Kenyatta ameagana na mwenyeji wake, Rais Magufuli katika Uwanja wa Ndege wa Chato.
Katika ziara hiyo, marais hao wamesisitiza kudumisha amani na uhusiano mzuri katika nchi za Jumuiya Afrika Mashariki na kushirikiana katika mambo mbalimbali ikiwemo biashara.
Ukizungumzia 'ushiriakiano wa kibiashara', ikumbukwe hivi karibuni mbunge wa starehe almaarufu kama Jaguar alizua gumzo mitandaoni baada kutangaza jaribio la kufukuzwa kwa wageni wote wanaofanya boashara nchini Kenya wakiwemo wafanyabiashara wa Tanzania hali ambayo haikuwa sawa katika mahusiano yetu na Kenya kibiashara.
Hivyo ziara yake hii, itakuwa imeleta matumaini mapya ya kushirikiana kibiashara kati ya Tanzania na Kenya.

Paskali Joseph
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIS KENYATTA AREJEA NYUMBANI NA MATUMAINI TELE
Reviewed by By News Reporter
on
7/07/2019 09:04:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: