Loading...

MFALME WA DUBAI AMFUMANIA MKEWE NA MLINZI WAKE

Loading...
Kulingana na vyombo vya habari, inataarifiwa kuwa mpasuko unazidi kutokea katika ndoa ya kiongozi mkuu wa Dubai, Sheikh Mahammed al Maktoum na mkewe bi. Haya.

Ametaarifu kuwa mwanamke wake amezidisha ukaribu na mlinzi wake wa nchini Uingereza hii ni baada ya kuwakuta pamoja baada ya kufanya ziara ya ghafla katika nyumba yao ya mjini London.

Chanzo cha karibu kutoka kwenye familia hiyo kinasema Sheikh 'alishtushwa' alipomfumania mlinzi wa mkewe katika mazingira ya kutatanisha na kumtaka mkewe arudi Dubai mara moja lakini mkewe huyo alikataa na kusema anajiandaa kwa talaka.

Sheikh alirudi nyumbani kwake Dubai - wakati mkewe akisalia nchini Uingereza na watoto wake.

Wawili hao tayari wote wanaelekea kufungua kesi mahakamani, ikiwa Mfalme anafungua kesi kwa ajili ya watoto ili waweze kurudishwa Dubai na Bi Haya kwa ajili ya talaka.

Bi Haya ni mkewe wa sita wa mfalme wa Dubai, juma lililopita iliripotiwa kukimbia na zaidi ya Bilioni 80 pesa za Tanzania na kukimbilia Ujerumani na baadae kurudi kwake Uingereza.
Na Richard Owino.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MFALME WA DUBAI AMFUMANIA MKEWE NA MLINZI WAKE MFALME WA DUBAI AMFUMANIA MKEWE NA MLINZI WAKE Reviewed by By News Reporter on 7/07/2019 10:34:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.