Loading...

RAPA NICKI MINAJ AHAIRISHA KUFANYA TAMASHA SAUDIA BAADA YA VIKWAZO VIKALI

Loading...
Mwanamuziki Nicki Minaj amelazimika kuvunja tamasha alotakiwa kulifanya nchini Saudi Arabia wiki ijayo akisema anaunga mkono haki za wanawake na wapenzi wa jinsia moja.

Taarifa za nyota huyo wa miondoko ya rap kutumbuiza Saudia ziliwashtua wengi na kusababisha kelele kali kutoka kwa wanaharakati wanaokosoa rekodi ya haki za binadamu ya nchi hiyo.

Wengine wakawa wanajiuliza msanii huyo atavaaje kwenye tamasha hilo kwa kuwa nchi hiyo inafuata mfumo wa kihafidhina wa Kiislamu, na Minaj ni maarufu kwa kuvaa nusu uchi.

Saudi Arabia imekuwa ikijaribu kulegeza vikwazo kwenye sekta ya burudani ili kukuza sekta ya sanaa kwa ujumla ya nchi hiyo.
Na Fatma Omari.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAPA NICKI MINAJ AHAIRISHA KUFANYA TAMASHA SAUDIA BAADA YA VIKWAZO VIKALI RAPA NICKI MINAJ AHAIRISHA KUFANYA TAMASHA SAUDIA BAADA YA VIKWAZO VIKALI Reviewed by By News Reporter on 7/10/2019 09:06:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.